“Tumeamua kuikubalia Jamhuri ya shirikisho la Somalia chini ya mkataba wa kujiunga na Jumuia,” mwenyekiti wa Jumuia hiyo anayemaliza muhula wake, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema katika mkutano wa Jumuia hiyo mjini Arusha, Tanzania.
Somalia ambayo Rais wake Hassan Sheikh Mohamud alikuwa kwenye mkutano, inaungana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.
Jumuia ya Afrika Mashariki yenye makao yake makuu mjini Arusha ambako mkutano huo ulikuwa unafanyika, ilianzishwa mwaka 2000, na inahusika na kuhimiza biashara kwa kuondoa ushuru wa forodha baina ya nchi wanachama.
Ilianzisha soko la pamoja mwaka wa 2010.