Baraza hilo lenye wanachama 15 lilipiga kura kwa kauli moja Ijumaa usiku kuunga mkono azimio lililoandikwa na Uingereza la kuondoa marufuku ya silaha. Hata hivyo, Ufaransa ilikuwa mwanachama pekee aliyejiweka kando wakati wa kupiga kura juu ya azimio jingine la kuweka tena marufuku ya silaha kwa wanamgambo wa al-Shabaab wenye uhusiano na al-Qaeda, ikisema azimio hilo halina marejeleo ya migogoro ya eneo kati ya Djibouti na Eritrea.
Katika taarifa iliyotumwa kwa Shirika la Habari la Associated Press, Waziri wa Habari Daud Aweis alisema kuondolewa kwa marufuku hiyo kutasaidia kuvifanya vikosi vya jeshi nchini humo kuwa vya kisasa. Somalia imekuwa ikikabiliana na changamoto kubwa za kiusalama, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa makundi yenye itikadi kali kama vile al-Shabab.
Serikali ya Somalia inahitaji kupata fursa ya kuwa na silaha na vifaa vya kisasa ili kukabiliana vilivyo na vitisho hivi na kudumisha usalama ndani ya mipaka yake ilisema taarifa hiyo.