Serikali ya Sudan Kusini Jumanne ilisema shule zitafunguliwa tena wiki ijayo baada ya kufungwa kwa wiki mbili kutokana na joto kali nchini kote.
Wizara za afya na elimu zilisema viwango vya joto vinatarajiwa kushuka sana huku msimu wa mvua ukitarajiwa kuanza siku zijazo.
Sudan Kusini katika miaka ya karibuni ilikumbwa na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa, huku joto kali, mafuriko na ukame vikiripotiwa katika misimu tofauti.
Wakati wa wimbi la joto wiki iliyopita, nchi ilirekodi viwango vya joto hadi nyuzi joto 45.
Taasisi za elimu ya juu ziliendelea kufungua milango.