RSF imekubali kuhudhuria mazungumzo ya Geneva ni juhudi ya kwanza kubwa ya upatanishi ya pande mbili zinazopigana Sudan.
Serikali ya Sudan imesema leo Ijumaa itapeleka ujumbe kwenda Jeddah kushauriana na Marekani kuhusu mwaliko wa mazungumzo ya kusitisha mapigano mjini Geneva yatakayofanyika Agosti 14.
Mazungumzo hayo yanalenga kumaliza vita vya miezi 15 kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF). Mazungumzo ya Geneva, ambayo RSF imekubali kuhudhuria, yatakuwa juhudi ya kwanza kubwa katika miezi ya upatanishi kati ya pande hizo mbili zinazopigana nchini Sudan.