Rwanda yaadhimisha miaka 20 tangu mauwaji ya halaiki

wasani wakiigiza baadhi ya matukio yaliyotokea wakiingia kwenye uwamja wa michezo kuadhimisha miaka 20 ya mauwaji halaiki kwenye uwanja wa  Amahoro, Kigali, April 7, 2014.

Bizimana Emmanuel, aliyezaliwa miaka miwili kabla ya mauwaji ya haliaki, anatulizwa na mwanamke asiyejulikana alipokua anahudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 20 katika uwanja wa mchezo wa Amahoro, Kigali, April 7, 2014.

Wasani wakicheza baadhi ya matukio ya mauwaji wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya mauwaji ya  Rwandan kwenye uwanja wa micehzo wa Amahoro Kigali, April 7, 2014.

Wanawake wawili wanaolia, ni miongoni mwa kadhaa walozidiwa na majonzi wakikumbuka ukatili ulotendeka wakati wa mauwaji ya halaiki wakibebwa kusaidiwa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 20 kwenye uwanja wa Amahoro Kigali, April 7, 2014.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki Moon, Rais Paul Kagame, wa Rwanda na mkewe Jeannette Kagame pamoja na mwenkiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika AU Nkosazana Dlamini-Zuma wanashiriki katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya mauwaji halaiki mjini Kigali, April 7, 2014.

Watoto wa Rwanda wasikiliza na kuomba dua wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la Saint-Famille Catholic, mahala ambapo watu wengi waliuliwa wakati ya mauwaji ya 1994 katika mji mkuu wa Kigali, April 6, 2014.

Waombolezi wa Kinyarwanda wakihudhuria ibada katika kanisa la Evangelical Restoration Church, Kimisagara, siku moja kabla ya kuadhimisha miaka 20 ya mauwaji ya 1994 mjini, April 6, 2014.

Picha za watu wa familia kadhaa walouliwa zikiwa zimetundikwa katika kituo cha makumbusho ya mauwaji halaiki ya Rwanda mjini Kigali, April 5, 2014.