Russia Alhamisi ilifanya shambulio kubwa sana la makombora katika maeneo kadhaa ya Ukraine, kwa kushambulia vituo vya umeme katika kile maafisa wamesema ilionekana kuwa shambulio la kwanza kubwa katika operesheni zake mpya dhidi ya mitambo ya umeme ya Ukraine.
Umeme ulikatika katika mikoa mitano upande wa magharibi, katikati na mashariki na kufufua kumbukumbu ya mashambulizi mengi ya anga kwenye miundombinu muhimu wakati wa msimu wa baridi kali, ambayo yalisababisha ukosefu wa umeme kwa mamilioni ya Waukraine katika kipindi cha baridi kali.
Maafisa wamesema takriban watu 18 walijeruhiwa katika mashambulizi ya anga, akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka 9, na gavana wa mkoa amesema watu wawili waliuawa katika shambulio tofauti la usiku.