Russia yadaiwa kupanga kufanya muundo mpya wa kiutendaji Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, Jumamosi imesema katika ripoti yake ya kijasusi ya  kila siku kuhusu Ukraine, kwamba kuna uwezekano Russia ikafanya muundo wa kiutendaji wa kujihami zaidi.

Hii ni baada ya matokeo yasiyo na uhakika kutokana na majaribio yake ya kufanya mashambulizi ya jumla tangu Januari 2023 nchini Ukraine.

Wanajeshi wa Ukraine wameingia Bakhmut badala ya kurudi nyuma.

Baadhi ya wataalam wa kijeshi wa magharibi wanasema mbinu hii inaweza kuwa hatari kwa sababu Ukraine inahitaji kuhifadhi vikosi kwa ajili ya mashambulizi.

Hatahivyo, kulingana na Uingereza, shambulio la Russia la Bakhmut limekwama.

Wakati huo huo, kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu inasema baadhi ya raia 10,000 wa Ukraine, wengi wao wazee au wana ulemavu, wamekuwa wakikabiliwa na mazingira magumu huko Bakhmut na makazi ya jirani.