Russia inadai kuwashikilia wanajeshi 1000 wa Ukraine

Your browser doesn’t support HTML5

Zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine wamejisalimisha katika mji wa bandari wa Mariupol, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema Jumatano.

Taarifa hii ni kufuatia mkakati wake mkubwa wa kuulenga mkoa wa Donbas mashariki mwa nchi, ambao umeharibiwa vibaya lakini bado hauko chini ya udhibiti wa Russia.