Rais wa zamani wa Honduras atarajiwa kuhamishiwa Marekani

Rais wa zamani wa Honduras Juan Orlando Hernandez

Rais wa zamani wa Honduras Juan Orlando Hermandez anatarajiwa kuhamishiwa Marekani.

Polisi walimkamata na kumfunga pingu wakiwa na nguo za kujikinga na risasi mbele ya waandishi wa habari jana kufuatia ombi la Marekani.

kukamatwa kwake kunakuja chini ya wiki tatu baada ya Hermandez kuondoka ofisini na kufuatia miaka ya shutuma za waendesha mashataka wa Marekani kwa kuhusika kwake na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Hermandez alihusishwa mara kwa mara na waendesha mashtaka wa New York, kama mmoja wa wahusika kwenye kesi ya biashara ya dawa za kulevya ya kaka yake mwaka 2019.

Kaka yake Juan Antonio anayejulikana kama Tony Hermandez alikutwa na hatia katika mashtaka ya dawa za kulevya na silaha na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Hermendez aliapishwa kuwa mwakilishi wa Honduruz katika bunge la Amerika ya Kati Januari 27 saa chache tu baada ya mrithi wake Xiomara Castro kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.

Wakili wake alisema ana kinga ya kuhamishwa kwa sababu ni mjumbe wa bunge la kieneo.