Kisha akapitia kwenye Disco Maghreb, duka la kihistoria na lebo ya wasanii wanaoimba muziki wa jadi nchini humo , ikiwa ni muingiliano mzuri katika safari ya Algeria iliyotawaliwa na diplomasia iliyo na utete.
Macron siku ya Ijumaa aliahidi kubadilika zaidi katika kutoa visa kwa Waalgeria baada ya mzozo mkubwa wa kidiplomasia kuzuka mwaka jana kati ya nchi hizo mbili kuhusu suala hilo.
Yeye na rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune pia walikubaliana kuunda tume ya pamoja ya wanahistoria ambao watachunguza siku za nyuma tangu mwanzo wa ukoloni wa Ufaransa mwaka 1830 hadi uhuru wa Algeria.
Ziara yake pia ililenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.