Qatar inasema mashauriano ya sitisho la mapigano Gaza yafikia hatua muhimu

  • VOA News

Waziri mkuu wa Qatar bin Abdulrahman Al Thani

Waziri Mkuu wa Qatar na Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al thani amesema leo kuwa mashauriano kwa sitisho jipya la mapigano huko Gaza yako katika ‘awamu nyeti.’

Aliwaambia wanahabari kuwa juhudi zinafanywa kuzungumzia vikwazo ili kuweza kufikia makubaliano.

Qatar, Misri na Marekani zimehusika katika mazungumzo ili kupata sitisho la mapigano ambalo pia huenda litaruhusu kujumuisha kuachiliwa kwa baadhi ya mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza na Israel kuwaachilia huru wafungwa wa Palestina wanaowashikilia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alijadili suala hilo katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Qatar jana Jumanne.