Polisi wakamata waandamanaji Kenya

Polisi watawanya maandamano Kenya

Wafuasi kadhaa wa muungano wa upinzani wakematwa na polisi katika miji tofauti nchini Kenya.

Wafuasi hao walijitokeza kushiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika kila Jumatatu na muungano wa CORD, kushinikiza makamishna wa tume ya uchaguzi kujiuzulu kwa madai ya kutowajibika kwa Umma.

Katika mji wa Mombasa, Gavana Ali Hassan Joho, ambaye ni naibu kinara wa chama kikuu cha upinzani nchini Kenya (ODM).

Gavana Joho, aliongoza maandamano waliyoyataja kama ya amani, lakini yakasitishwa na polisi wa kutuliza ghasia.

Mwandishi wetu Josephat Kioko alishuhudia maandamano hayo, na alituma taarifa ambayo unaweza kuisikiliza hapo chini.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Josephat Kioko kuhusu maandamano ya Mombasa.