Polisi wa Kenya wachelewa kufika Haiti

Polisi wa Kenya wakishika doria katika mitaa ya Nairobi, Kenya. Nchi hiyo ilikubali mwezi Oktoba kuongoza jeshi la polisi la kimataifa lililoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kwenda Haiti, lakini Mahakama Kuu ya Kenya Januari iliamua mpango huo kuwa kinyume na katiba,

Maafisa wa Marekani walidokeza  kuwa maafisa  wa polisi wa Kenya watakuwa Port-au-Prince nchini Haiti kufikia Alhamisi ili wawe sanjari na ziara ya kitaifa ya Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Marekani.

Maafisa wa Marekani walidokeza kuwa maafisa wa polisi wa Kenya watakuwa Port-au-Prince nchini Haiti kufikia Alhamisi ili wawe sanjari na ziara ya kitaifa ya Rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Marekani.

Lakini upelekaji wa maafisa hao wa polisi nchini Haiti kuongoza kikosi cha kimataifa cha kupambana na magenge umecheleweshwa baada ya safari ya ndege iliyopangwa kutoka Nairobi kuahirishwa siku ya Jumanne, vyanzo viwili vilivyoarifiwa kuhusu suala hilo viliambia Reuters.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Marekani Joe Biden, Ruto alirejea kuelezea nia ya dhati ya Kenya kuwapeleka maafisa hao nchini Haiti.

Kenya ilijitolea mwezi Julai kuongoza ujumbe wa kwenda huko lakini imekuwa ikikabiliwa na uchelewesho wa mara kwa mara wa kwenda huko kutokana na kesi zilizoletwa na wapinzani wa mpango huo wa serikali na kuongezeka kwa ghasia mwezi Machi zilizopelekea Waziri mkuu wa Haiti kujiuzulu.