Ofisi za UN zavamiwa nchini Burundi

Francoise Hampson, Fatsah Ouguergouz and Reine Alapini Gansou, wajumbe wa Tume ya inayoichunguza Burundi huko Geneva, Switzerland.

Kundi la watu wenye silaha walivunja ofisi za ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa mjini Bujumbura, nchini Burundi mapema leo.

Tukio hilo limetokea wiki moja baada ya tume hiyo kuripoti uwezekano wa uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Burundi, ikijumuisha mauaji na kukamatwa watu kiholela, utesaji, udhalilishaji wa kijinsia na kupotea kwa watu.

Nchi hiyo imekuwa katika hali ya taharuki ya kisiasa toka rais wa nchi hiyo Piere Nkurunzinza kugombea na kushinda kipindi cha tatu cha muhula wa urais wenye utata mwaka 2015.

Hakukuwa na taarifa yoyote kuhusiana uharibifu ama madhara kutokana na uvunjwaji huo wa ofisi.

Your browser doesn’t support HTML5

Shambulizi la ofisi za UN Burundi