Ofisi za mawakili wa Mbabazi zavamiwa

Ofisi mbili za mawakili wa aliyekuwa mgombea wa Urais nchini Uganda, Amama Mbabazi, zimevunjwa usiku wa kuamkia Jumatano.
Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wetu Kennes Bwire, aliyeko Kampala, Uganda, vitu vilivyoibiwa ni pamoja na tarakilishi na karatasi zinazoelezwa kuwa na ushahidi muhimu.
Nyaraka hizo ni za kesi ya Amama Mbabazi aliyoifungua mahakamani ambayo ipo hivi sasa kupinga ushindi wa Rais Yoweri Museveni, katika uchaguzi wa mwezi Februariu.
Mbabazi anadai kuwa na ushahidi wa kutosha kwamba polisi 30 kutoka kituo cha polisi cha Wandegeya, jijini Kampala, ndio waliotekeleza uvamizi huo.
Ushahidi huo unadai nia ni kumsaidia Rais Museveni kupata ushahidi walio nao na kudhibitisha kwamba uchaguzi uligubika udanganyifu katika hesabu ya kura.
Pamoja na madai hayo kutolewa, polisi baso wamesalia kimya.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya mwandishi wetu wa Kampala, Uganda, Kennes Bwire ya kuvamiwa kwa ofisi za Mawakili wa Amama Mbabazi.