Picha za Novemba 25 , 2015.

Mfanyakazi wakujitolea amshika mtoto wakati wenzake wanaposaidia wahamiaji na wakimbizi kushuka kwa mtumbwi baada ya kuwasili kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos.

 Papa Francis asalimia watumbuizaji wa kitamaduni baada ya kushuka ndege kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, Kenya.

 Mwanaume awekelea mauwa kwenye gari la polisi karibu na basi lililoshambuliwa na wanamgambo mjini Tunis ,Tunisia na kuuwa watu 13.

 Maji yamwagika kutoka kwa ndoo katika juhudi ya kuzima moto mkubwa uliotokea kwenye kijiji cha Mandaluyong,mashariki mwa Manila, Ufilipino.

Daraja ya Mimico karibu na bustani ya Humber ilioko Toronto, Canada.

 Watu wasaidia kumuinua farasi aliebebeshwa mizigo kupita kiasi katika kitongoji cha  Peshawar, Pakistan.

Gari likiwa limezama baada ya mvua kubwa zilizosababisha mafuriko Riyadh, Saudi Arabia.

 Mji mku wa Bangkok Thailand.

Jua laanza kuchomoza baada ya kipindi cha kuanguka ka theluji karibu na mji wa Baxter, California.