Nigeria yaanza vibaya katika kikapu kwenye michuano ya olimpiki

Mchezaji wa Nigeria Josh Okogie kushoto akimpita Matisse Thybulle wa Australia katika mchezo wao wa mchuano wa Olimpiki huko Tokyo Japan Jumapili July 25.

Wawakilishi wa Afrika katika michuano ya Olimpiki ya mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume Nigeria Jumapili walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuangukia pua mbele ya Australia kwa jumla ya pointi 84-67.

Katika mchezo huo Patty Mills aliiongoza Australia kwa kupachika jumla ya pointi 25.

Na kwa upande wa Nigeria Obi Emegano anayecheza katika timu ya Fuenla-brada ya ligi ya Uhispania ACB aliiongoza Nigeria kwa kupachika jumla ya pointi 12.

Nayo timu ya Ufaransa iliwashangaza Marekani kwa kuwaangusha miamba hao wa kikapu kwa jumla ya pointi 83-76, kushindwa huko ni kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo kwa Marekani tangu mwaka 2004 huko Athens katika michuano ya Olympik.

Jryu Holiday wa Milwaukee Bucks aliongoza timu ya Marekani kwa kupachika pointi 18 , katika mchezo huo na kwa upande wa Ufaransa Evan Fournier aliongoza kikosi chake kwa kupachika pointi 28.