Melfu ya waandamanaji wamejitokeza barabarani mjini Jerusalem kupinga mapendekezo ya Netanyahu kupunguza nguvu za majaji, hatua ambayo wakosoaji wake wanasema utadunisha mfumo wa demokrasia wa Israel.
Wabunge waliujadili mswaada huo jumapili, hadi usiku.
Polisi wametumia maji kuwatawanya mamia ya waandamanaji waliofunga lango kuu la kuingia bungeni, leo Jumatatu.
Netanyahu anatarajiwa bungeni wakati wa upigaji kura kuhusu mswaada huo, licha ya kwamba ametoka hospitali siku chache zilizopita ambako aliwekewa kifaa cha kusaidia moyo wake kufanya kazi.
Miongoni mwa maswala yenye utata kwenye mswaada huo ni kupunguza uwezo wa mahakama kuu kubadilisha maamuzi ya bunge, pamoja na kubadilisha mchakato wa kuteua majaji.