myanmar holds historic election

wafuasi wa chama cha National League for Democracy party wakifurahia wakati wa kusubiri matokeo ya uchaguzi nje ya makao makuu ya NLD huko Yangon, Myanmar, Nov. 8, 2015.

Afisa kutoka tume ya uchaguzi ya Myanmar akionyesha kura zilizopigwa katika uchaguzi mkuu  Yangon, Nov. 8, 2015.

Waislamu wakiwa wamesimama katika mstari kupiga kura zao nje ya kituo cha kupigia kura huko Mandalay, Nov. 8, 2015.

Rais wa Myanmar Thein Sein akipiga kura huko Naypyitaw, Nov. 8, 2015.

Sein Kyi, mwenye umri wa miaka 87, na familia yake wakionyesha vidole vyao vyenye wino baada ya kupiga kura Yangon, Nov. 8, 2015.

kiongozi wa chana cha National League for Democracy (NLD) party Aung San Suu Kyi akiwasili katika kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Wafuatiliaji wa uchaguzi kutoka jumuiya ya ulaya wakiwa katika kituo cha kupigia kura huko Yangon  Yangon, Nov. 8, 2015.

Mwanamke akipiga kura katika kituo wakati wa uchaguzi mkuu huko Yangon, Nov. 8, 2015. 

wanawake wakitafuta majina katika daftari la wapiga kura kwenye kijiji cha Dala, Nov. 8, 2015.

wafanyakazi wa kujitolea wakiandaa vifaa vya kupigia kura katika kituo cha Dala .

mmoja wa raia wa kawaida elfu 40,000 akiwa amevalia kama polisi maalumu kwa ajili ya kusaidia masuala ya usalama kwenye vituo vya kupigia kura.

Mfanyakazi katika kituo cha kupigia kura akikagua kura safi katika kituo cha Yangon, Nov. 8, 2015.

Mpiga kura mzee akiwa anasaidiwa kufika katika kituo chake ili kupiga kura yake Nov. 8, 2015.

Watu wakiwa wamesimama nje ya kituo cha kupigia kura huko Mandalay, Nov. 8, 2015.