Mwili wa Rais mstaafu wa Marekani ukiagwa kwenye ukumbi wa Bunge la Marekani

Jeneza la aliekuwa Rais wa Marekani, George W.H Bush, likiwasili katika ukumbi wa Rotunda, Washington, D.C., Desemba. 3, 2018.

Rais wa Marekani Donald J. Trump, akiwa na mkewe wake Melania Trump, akipiga saluti kuonyesha heshima kwa mwili wa Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush katika chumba cha Rotunda kilichoko katika Bunge la Marekani Washington, DC, Desemba 3, 2018

 

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, wakiwasili kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Rais mstaafu George H. W. Bush ukiwa katika ukumbi wa Rotunda, ndani ya Bunge la Marekani, Jumatatu, Dec. 3, 2018 , Washington. (Brendan Smialowski/Pool via AP)
 

Mwanajeshi wa jeshi la majini kutoka manuari ya kivita ya USS George H.W. Bush akiwa anaangalia ndege iliyokuwa imebeba jeneza lenye mwili wa Rais mstaafu George H.W. Bush arrives katika kituo cha jeshi la anga ( Andrews Air Force Base), Maryland, Desemba. 3, 2018.

Sully, mbwa msaidizi wa Rais mstaafu wa Marekani George H.W Bush, akiwa amesimama pembeni ya familia ya Bush katika kituo cha kijeshi cha Andrews huko Maryland, Desemba3,  2018.

Watu waliojitokeza kuja kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Rais mstaafu wa Marekani George H.W. Bush ulioko katika jeneza lililofunikwa na bendera ya Marekani uliokuwa umewekwa katika ukumbi wa Rotunda, Washington, Jumanne, Desemba. 4, 2018. (AP Photo/Patrick Semansky)

Kutoka kushoto, Makamu wa Rais mstaafu Dan Quayle, Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu James Baker III, Makamu wa Rais mstaafu Dick Cheney, na Waziri wa Mambo ya Nje mstaafu Colin Powell, wakiwasili katika ukumbi wa Rotunda, ulioko katika bunge la Marekani, Washington, kuhudhuria shughuli za kuuwaga mwili wa Rais mstaafu George H.W. Bush.

Jeneza la aliekuwa  Rais wa Marekani

Makamu wa Rais Marekani, Mike Pence, Rais wa zamani wa Marekani, Geoge W.Bush, ,na Mkee wake Laura Bush, wakiangalia  jeneza lenye mwili wa Rais wa Zamani wa Marekani Geouge H. W Bush ndani ya jengo la Capitol, Washington DC, Dec 3, 2018

Bendera ya Marekani ikipepea nusu mlingoti, katika maombolezi ya kifo cha Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush, Washington, Desemba 3, 2018.
 

Waombolezaji watoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa Rais George H.W. Bush ambao umelazwa kwa heshima za kitaifa katika ukumbi wa bunge la Marekani