Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ategua bomu katika mji mkuu wa Uturuki na kujiua

Ramani ya miji ya Uturuki ya Istanbul na Ankara

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga alitegua bomu katika mji mkuu wa Uturuki Jumapili, karibu na jengo la wizara ya mambo ya ndani, na kujiua na kujeruhi maafisa wawili wa polisi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki alisema mshambuliaji wa pili aliuawa katika majibizano ya risasi na polisi, shirika la habari la Associated Press limeripoti.

Mlipuko huo ulitokea saa chache kabla ya bunge kuanzisha tena shughuli zake baada ya mapumziko ya miezi mitatu. Akilihutubia bunge, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo akisema "wanaotishia usalama na amani ya wanainchi bado hawajafikia malengo yao na hawatoyafikia kamwe."

Kundi la wapiganaji wa Kikurdi limekiri kuhusika na shambulio hilo.