Morsi afunguliwa mashtaka zaidi

Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi wa kundi la Muslim Brotherhood mjini Cairo, Jan. 8, 2014.

Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi tayari anashtakiwa kwa shutuma za kuchochea ghasia pia atashtakiwa kwa makosa ya kuidhalilisha mahakama.

Your browser doesn’t support HTML5

Sikiliza sauti ya ripoti hii


Shirika la habari la Misri liliripoti jumapili kwamba muda mfupi kabla ya jeshi kumuondoa madarakani bwana Morsi alimshutumu jaji mmoja wa uchaguzi kwa wizi wakati wa hotuba yake.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano ya Esther Githui-Ewart na Ismail Mfaume wa Misri


Rais huyo wa zamani tayari amefunguliwa mashtaka kwa kuchochea ghasia ambazo zimesababisha vifo vya waandamanaji. Pia anakabiliwa na kesi nyingine mbili, moja kwa shutuma za upelelezi na nyingine kwa kuandaa mpango wa kuvunja gereza moja. Viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood la bwana Morsi pia wanakabiliwa na mashtaka kama hayo.

Jeshi la Misri lilimuondoa madarakani bwana Morsi mwezi Julai wakati upinzani ulipomshutumu kwa kujilimbikizia madaraka mengi. Wamisri walipiga kura kwa kauli moja kuunga mkono kura ya maoni wiki iliyopita ili kupitisha katiba mpya ambayo itachukua nafasi ya ile ambayo inaungwa mkono na wafuasi wa bwana morsi. Uchaguzi wa rais mpya na wabunge unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.