Obama kuhudhuria mkutano wa NATO

Rais Obama akitoa hotuba, mjini Warsaw

Rais wa Marekani, Barack Obama, anahudhuria mkutano wa siku mbili unaoelezwa ni muhimu kabisa wa viongozi wa NATO tangu kumalizika kwa vita vya itikadi mjini Warsaw hii leo Ijumaa.

Suala kuu kwenye ajenda ya mazungumzo hayo ni kutaka kujiondowa kwa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya, pamoja na wasiwasi juu ya kile kitakachotendeka kutokana na kujiondoa kwa mshirika wa NATO mwenye nguvu Uingereza kutoka Umoja huo.

Rais Obama amesema Marekani inamaslahi makubwa na ya muda mrefu katika Ulaya iliyoungana na kila mmoja anahaja ya kupunguza msukosuko wowote wakati EU inapanga ushirikiano mpya.

Kiongozi huyo wa Marekani anatarajiwa kuwahakikishia viongozi wa Ulaya wakati wasiwasi ukiwa unaongezeka barani humo, juu ya mustakbali wa kuungana kwa Ulaya baada ya Brexit