Mke wa raia wa Iran ambaye ni pia ni Mswidi Ahmadreza Djalali anayeshutumiwa kwa ujasusi na kutishiwa kunyongwa nchini Iran, siku ya Jumamosi alitoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuhakikisha mume wake anaachiliwa huru.
"Natumai kwamba EU inaweza kweli kuchukua hatua madhubuti ili kumrudisha Ahmadreza nyumbani," Vida Mehrannia alisema kulingana na sehemu ya mahojiano kwenye idhaa ya ZDF ya Ujerumani.
EU lazima "isiruhusu mtu asiye na hatia kuuawa kwa njia hiyo ya kinyama", aliongeza.
Djalali alihukumiwa kifo mwaka 2017 kwa tuhuma za ujasusi, tuhuma zilizokanushwa na Sweden na wafuasi wake.