Muungano wa vyama vya wafanyakazi wa viwanda vya magari Marekani, (UAW) uliongeza mgomo wake dhidi ya viwanda vikubwa vitatu vya magari vya Detroit, Jumatano kwa kunaza mgomo kwenyen tawi la kiwanda cha malori cha Ford, cha Louisville, Kentucky.
Katika hali ya mshangao, wanachama 8,700 walisimama kufanya kazi zao saa 6:30 mchana kwenye kiwanda ambacho hutengeneza magari makubwa ya kubeba mizigo ya F-Series na magari makubwa yaani SUV.
Rais wa UAW, Shawn Fain, amesema katika taarifa kwamba muungano huo umesubiri kwa muda wa kutosha, lakini Ford haijatoa ujumbe wa kujadiliana kuhusu mikataba ya haki.
Ford iliuita mgomo huo kuwa si uwajibikaji, lakini ikasema haishangazwi kutokana na taarifa za uongozi wa UAW, kwamba ulitaka kuweka kiwanda hicho kwenye hali mbaya.