Jopo la majaji watatu kwenye mahakama ya Barcelona wamemkuta na hatia Alves mwenye umri wa miaka 40 kwa tukio lililofanyika Desemba 31, 2022. Kando na kifungo hicho, mahakama pia imemuamuru kulipa fidia ya dola 162,000 kwa muathirika. Pia amepigwa marufuku kukaribia nyumba yake wala mahala pake pa kazi, huku mawasiliano yote yakisitishwa kwa miaka 9.
Alves ambaye alikuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo alionekana mtulivu, kulingana na wakili wake Ines Guardiola. Davis Saenz ambaye ni kutoka upande wa muathirika amesema kwamba wameridhishwa na uamuzi huo, ambao umethibitisha kuwa muathirika alikuwa akisema kweli tangu mwanzo.
Wakili wa muathirika Ester Garcia awali waiki hii alisema kwamba yeye na mteja wake hawatafika mahaka hivi leo, wakati wa kutolewa hukumu hiyo.