Mazungumzo ya amani huko Burundi yatafanyika baadae mwezi huu

Willy Nyamitwe, msemaji wa serikali ya Burundi.

Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi yaliyokuwa yafanyike Jumatatu mjini Arusha nchini Tanzania chini ya mpatanishi wake Rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa yameakhirishwa tena.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na msemaji wa serikali ya Burundi, Willy Nyamitwe ambaye alisema kwamba serikali ya Burundi ilipokea taarifa ya kuakhirishwa mazungumzo hayo iliyoeleza kwamba hatua hii itatoa muda zaidi wa ushauri na washika dau na vyama vyote vyenye wasiwasi.

Your browser doesn’t support HTML5

Mahojiano ya VOA na msemaji wa serikali ya Burundi, Willy Nyamitwe

Kulikuwa na matumaini kwamba kuteuliwa kwa mpatanishi mpya wa kieneo katika mgogoro wa Burundi kutaharakisha utaratibu wa amani. Hivi sasa mazungumzo hayo ya upatikanaji amnai huko Burundi yanatarajiwa kufanyika baadae mwezi huu wa Mei.