Mazishi ya Maalim Seif Sharif Hamad Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Mwinyi na (kushoto)Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleimn Andulla na (kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Idrisa Kitwana Mustafa na Viongozi wengine wa Serikali na Chama wakiupokea Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ulipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amari Karume Jijini Zanzibar, kwa ajili ya kuangwa na Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnazi mmoja na kusafirika kwenda Pemba kwa maziko leo jioni.

Mwili wa Marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ukishushwa katika Helikota ya JWTZ baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar ukitokea Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Samia akijumuika na wananchi wa Zanzibar katika sala ya kuuaga mwili wa  Maalim Seif.

Makamu wa Rais Samia akijumuika na wananchi wa Zanzibar katika sala ya kuuaga mwili wa  Maalim Seif.

Maelfu wahudhuria mazishi ya marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.

Maelfu wahudhuria mazishi ya marehemu Maalim Seif Sharif Hamad.

Wananchi wa Zanzibar wahudhuria mazishi ya Maalim Seif.

Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi mwaka 2015.

Seif Shariff kiongozi wa ACT apiga kura Garagara, Zanzibar Oktoba 2020

Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, amezikwa Alhamisi kijijini kwao, Mtambwe Nyali Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar.