Mashirika ya kiraia Beni yawataka raia wasilipe kodi kwa serikali ya DRC

Eneo la Beni, Kivu kaskazini huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC

Mashirika ya kiraia huko Beni, Lubero na Butembo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC yamewataka wananchi wasilipe kodi yoyote ya serikali hadi kiongozi wa jeshi la Congo FARDRC atakapo tembelea eneo la Beni na kujionea mwenyewe hali ya kiusalama ilivyo na kusitisha mauwaji ya watu kote eneo la Beni na Lubero.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Austere Malivika akiwa Goma huko DRC

Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo baada ya mkutano uliofanyika katika mji wa Butembo ambapo mashirika yalikutana kufuatia mgomo wa siku tatu, bwana Kizito Binhangi alisema “ndio tunakuhakikishia tulimwandikia rais barua baada ya kuona kwamba mauaji yameendelea kwenye eneo hilo na ndio maana waliwataka wakazi wasilipe kodi yeyote kwa ni hawawezi kufanya hivyo huku wanashikiliwa”.
Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao huko Butembo ambako
mashirika yote yalikutana baada ya kufanyika mgomo huo mwishoni mwa wiki.