Marekani yatangaza ufadhili wa kijeshi wa  dola milioni 500 kwa Ufilipino

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipotembelea Mgahawa wa Auro katika Jiji la Taguig, Metro Manila, Ufilipino, Julai 30, 2024. REUTERS

Marekani imetangaza ufadhili wa kijeshi wa  dola milioni 500  kwa Ufilipino siku ya  Jumanne wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje,  Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin nchini humo.

Marekani imetangaza ufadhili wa kijeshi wa dola milioni 500 kwa Ufilipino siku ya Jumanne wakati Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin walipokutana na viongozi mjini Manila ili kuimarisha ushirikiano katika masuala kama vile uhuru wa usafiri na usalama wa mitandao.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa wanahabari baada ya mazungumzo na wenzao wa Ufilipino, Austin aliuita ufadhili huo uwekezaji wa kipekee wa kizazi kizima kusaidia kuvifanya vikosi vya jeshi la Ufilipino kuwa vya kisasa.

Waziri wa Ulinzi wa Ufilipino Gilberto Teodoro Jr. alisema uwekezaji wa kijeshi utaongeza hali ya ulinzi ya nchi hiyo na kusaidia kuzuia "uchokozi usiotakiwa na usio halali."