Marekani kunyima baadhi ya wahamiaji ukazi wa kudumu

Wahamiaji wakiwa kwenye kituo cha uhamiaji jimboni Texas

Mahakama ya juu ya Marekani Jumatatu imekataa kuruhusu wahamiaji 400,000 kutoka nchi12  kuishi  Marekani kwa sababu za kibinadamu kwamba hawastahili kupewa ukazi wa kudumu.

Kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters, uamuzi huo ni kutokana na rufaa iliyowasilishwa na mke na mme kutoka El Salvador, ambao walipewa hifadi ya muda lakini wakanyimwa vibali vya kuishi marekani kutokana na kuwa waliingia kwa njia isiyo halali mwanzoni.

Uamuzi huo huenda ukaathiri wahamiaji wengi walioishi Marekani kwa muda mrefu wakati wakitumia vibali vya muda. Licha ya rais mpya wa Marekani Joe Biden kubatilisha misimamo kadhaa ya mtangulizi wake Donald Trump kuhusiana na sera za uhamiaji, anaonekana kukubaliana na mahakama huhusiana na uamuzi wa jana.

Suala ambalo huenda likazua malalamishi kutoka kwa wanaharakati wa uhamiaji baadhi wakiwa ni kutoka chama chake cha Demokatik.

Mtayarishaji - Harrison Kamau