Marais wastaafu Marekani wahudhuria ibada ya kumuaga Barbara Bush

Wajukuu wa marehemu Barbara Bush wakibeba jeneza lake wakati wa ibada ya maziko yake huko Houston, Texas Aprili 2018.

Rais wa mstaafu Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakisalimiana na Melania Trump wakati wa ibada ya kumuaga marehemu Barbara Bush huko Texas, Aprili 21, 2018 

Rais mstaafu George W. Bush na baba yake Rais mstaafu George H. W. Bush wakiliangalia jeneza la Barbara Bush likipakiwa katika gari ya farasi nje ya kanisa la Mtakatifu Martin Aprili 21, 2018 huko mjini Houston. 

Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush akitoa hotuba ya rambirambi katika ibada ya maombolezo ya kifo cha mama yake, mke wa Rais wa Zamani Geroge H.W Bush April 21, 2018. 

Picha mbalimbali za marehemu Barbara Bush zikiuenzi uhai wake(1925-2018) 

Umati mkubwa wa watu waliohudhuria ibada maalum ya maziko ya Barbara Bush

Watu wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Barbara Bush

Hillary Clinton na mumewe Rais mstaafu Bill Clinton wakiwasili katika ibada ya kumuaga arrive at Barbara Bush. 

Mke wa Rais Trump, Melania Trump akiwasili katika ibada ya kumuaga marehemu Barbara Bush 

Ibada ya kumuaga marehemu Barbara Bush imefanyika Jumamosi katika Kanisa la Mtakatifu Martin Episcopal kwenye mji wa Houston, Jimbo la Texas.