Mambo yaliyojiri baada ya Bobi Wine kushikiliwa na vyombo vya usalama Uganda

Wakenya wafanya maandamano ya kupinga kushikiliwa kwa Robert Kyagulanyi- Bobi Wine katika jela ya kijeshi nchini Uganda

Wakenya wakiandamana mjini Nairobi.

Wakenya wakionyesha mshikamano na wananchi wa Uganda kupinga kushikiliwa kwa Robert Kyagulanyi- Bobi Wine.

Wakenya wafanya maandamano ya kupinga kuwekwa kizuizini kwa Robert Kyagulanyi- Bobi Wine

Mbunge maarufu wa upinzani wa Uganda Robert Kyagulanyi anayejulikana kama Bobi Wine (C) akiwa anaelekea katika  mahakama ya kijeshi, Gulu, kaskazini mwa Uganda, Agosti 23, 2018.

Mbunge maarufu wa upinzani wa Uganda Robert Kyagulanyi anayejulikana kama Bobi Wine (C) akiwa katika mahakama ya mwanzo huko Gulu, kaskazini mwa Uganda, Agosti 23, 2018

Mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi amefunguliwa mashtaka upya Alhamisi na serikali ya Rais Yoweri Museveni nchini Uganda kwa kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya uhaini.