Mahakama moja ya Misri ilimhukumu aliyekuwa mgombea urais mtarajiwa Ahmed Tantawy siku ya Jumatatu kifungo cha mwaka mmoja jela na kazi ngumu kwa tuhuma za kugushi nyaraka za uchaguzi, na kuzuiliwa kugombea katika uchaguzi kwa miaka mitano ijayo, wakili wake Khaled Ali alisema.
Tantawy alikuwa mwanasiasa mashuhuri zaidi kumpinga Rais Abdel Fattah al-Sisi alipokuwa akiwania muhula wa tatu mwaka jana.
Tantawy alisitisha kampeni yake akisema makundi yenye uhusiano na serikali yamemzuia kukusanya idadi inayohitajika ya uidhinishaji wa umma ili kujiandikisha kama mgombea, na kwamba darzeni ya wanafamilia na washirika wake wamekamatwa.
Mamlaka ilikanusha mchezo mchafu, na kumshtaki kwa ukiukaji unaohusishwa na hatua ya kampeni yake kusambaza nakala zao za fomu za kupata idhini.