Lungu ashinda tena kwenye uchaguzi wa Zambia

Rais Edgar Lungu akihutubia wafuasi wake awali wakati wa kampeni mjini Lusaka.

Uchaguzi wa Zambia umetangazwa Jumatatu huku Rais Edgar Lungu akichaguliwa tena kuwa Rais wa nchi hiyo.

Uchaguzi wa Zambia umetangazwa Jumatatu huku Rais Edgar Lungu akichaguliwa tena kuwa Rais wa nchi hiyo. Lungu wa chama cha Patriotic Front aliweza kujipatia kura 1,860,877 ikiwa ni asilimia 50.35 ya kura zilizopigwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu Hakainde Hichilema wa chama cha United Party for Democratic Development, UPND aliepata kura 1,760,347 ikiwa ni asilimia 47.67 ya kura zilizopigwa.

Your browser doesn’t support HTML5

zambia elections

Hata hivyo upande wa Hakainde umekataa matokeo hayo kwa madai kuwa uchaguzi huo ulikuwa umeibiwa. Wakili wa chama hicho cha upinzani cha UPND Jack Mwiimbu amesema watawasilisha malalamishi kwenye mahakama ya kikatiba akisema kuwa anaamini swala hilo litaangaliwa bila mapendeleo.

Harrison Kamau wa VOA alizungumza na mchambuzi Mkali Ephraim akiwa Lusaka, Zambia ambae alieleza hali ilivyo nchini humo.

Bonyeza usikilize.