Kumbukumbu ya shambulizi la Septemba 11

Eneo la south reflecting pool la Kumbukumbu ya Septemba 11 Memorial Plaza linaonekana katika maadhimisho ya miaka 10 ya kukamilika juhudi za awali za kusafisha eneo la tukio (Ground Zero) lilipoanzia huko New York, Mei 30, 2012. REUTERS/Andrew Burton

Wardi likiwekwa katika nakshi ya jina lililoandikwa katika eneo la South reflecting pool kwenye eneo la kumbukumbu - Ground Zero - katika hafla iliyotengwa rasmi kwa ajili ya Makumbusho ya Kumbukumbu ya Kitaifa ya Septemba 11 New York, Mei 15, 2014.

Kumbukumbu na Makumbusho ya Septemba 11, iliyopigwa picha katika eneo la maghorofa pacha yaliyoshambuliwa, New York, Aprili 23, 2021. Jengo refu limekalia pale yalipokuwa maghorofa pacha (Twin Towers) katika anga la New York. Ghorofa la One World Trade Center, lililofunguliwa 2014, limekuwa ni alama ya taifa la Marekani kujizatiti tena baada ya shambulizi la kutisha la Septemba 11.

Eneo la south pool la Kumbukumbu ya Septemba 11 linaonekana huku watalii wakitembelea ground zero huko New York  Juni 5, 2012.

Maafisa wa polisi wako nje ya eneo la Ground Zero asubuhi ya maadhimisho ya miaka 15 ya mashambulizi ya Septemba 11 huko Manhattan, New York, Marekani, Septemba 11, 2016. REUTERS/Andrew Kelly

Wasafiri wakipita katika kituo cha usafiri cha Oculus huko New York, Julai 30, 2021. Paa la jengo hilo hufunguliwa kila Septemba 11 ikiwa ni kuwaenzi wahanga wa mashambulizi ya Septemba 11.

Kituo cha usafirishaji cha Oculus Kiko pembeni ya Mnara wa Uhuru mjini New York, Julai 30, 2021. 

Hii picha inaonyesha ghorofa refu la One World Trade Center huko New York siku ya Julai 3, 2016, ni jengo refu lilikalia mahali palipokuwa maghorofa pacha (Twin Towers) katika anga za New York. Lilifunguliwa 2014.

Ghorofa la One World Trade Center "Freedo Tower" likionekana kuwa refu zaidi katika anga za mji wa Manhattan, New York, Juni 10, 2021.

Kumbukumbu hiyo ilifunguliwa katika eneo la maghorofa pacha ya World Trade Center. Makumbusho hayo yamejengwa katika eneo la moja ya maghorofa hayo na kufunguliwa Septemba 11, 2011, ili umma uweze kutembelea . Inawaenzi wale wahanga wote wa shambulizi la Septemba 11, 2001.