#voa400: Kubatizwa kwa watumwa kutoka Angola

Kwa mujibu wa ofisi ya Makumbusho ya Utumwa ya Taifa, Angola, watumwa walibatizwa kabla ya kusafirishwa kwenda Marekani. Kwa kuwabatiza, Kanisa Katoliki liliwavua mateka hao utambulisho wao wa Kiafrika.” -

Mwaka 1619, Meli ya Ulaya iliwasili katika koloni la Virginia na mzigo uliyokuwa haujategemewa. Mateka hawa, walikuwa wanatokea sehemu ambayo hivi leo ni nchi ya Angola.

“Biashara hiyo ya utumwa ilidhoofisha jamii za Kiafrika. Ilikuwa haiwezekani wakati wa biashara ya utumwa na ukoloni kwa jamii za Kiafrika kuweka sawa mifumo yao ya kisiasa na ufanyaji kazi.

Na wakati mwengine, watu wanajaribu kusahau sehemu hii ya historia ya nchi, na ndiyo sababu Makumbusho ya Utumwa imekuwepo," ameeleza Vlademiro Fortuna, Mkurugenzi, Makumbusho ya Utumwa ya Taifa Angola.