Kuachiliwa kwa Paul Rusesabagina, kutoka gereza la Rwanda Ijumaa jioni ni matokeo ya mashauriano ya miezi kadhaa kati ya Washington na Kigali.
Ambapo pande zote zikiwa na shauku ya kuweka sawa mambo ya kile walichokitaja kama kudhoofisha uhusiano wao.
Maafisa wawili wa Marekani mmoja kutoka kwa utawala wa rais Joe Biden, na msaidizi wa bunge walisema hakuna makubaliano kamili yaliyofikiwa ili kuachiliwa kwa Rusesabagina.
Rusesabagina ni mkazi wa kudumu wa Marekani ambaye umaarufu wake umetokana na hadithi yake katika filamu ya Hotel Rwanda ya 2004, ya kuwaokoa Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994.
Alikamatwa mwaka 2019 na baadaye kukutwa na hatia kwa mashtaka manane ya ugaidi yaliyotokana na nafasi yake kama uongozi katika Chama cha Rwanda Movement for Democratic Change (MRCD), ambacho kitengo chake chenye silaha, National Liberation Front (FLN), kiliishambulia Rwanda.