Kremlin yasema Putin yupo tayari kwa mazungumzo ya kumaliza vita

  • VOA News

Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin.

Kremlin imesema leo Ijumaa rais wa Russia Vladimir Putin yupo tayari kwa mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema kwamba Russia ina malengo yake yanayohusiana na usalama wake wa kitaifa na maslahi ya taifa, na kwamba ipo tayari kuhakikisha kwamba malengo yake yanatimia kupitia mazungumzo.

Elon Musk

Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Elon Musk kuhusu madai ya ufisadi nchini Ukraine, Peskov amesema kwamba watu wachache wana msimamo tofauti kuhusu yanayoendelea katika utawala wa Kyiv ambao hautaki mazungumzo ya amani na hautaki kuweka amani na kwamba wachache wana maoni tofauti yanayoambatana na matamshi yenye hisia.
Peskov amesema kwamba hakuna taarifa zaidi kuhusu uwezekano wa kufanyika mkutano kati ya rais Donald Trump na Putin, nchini Saudi Arabia.