Korea kaskazini yafanya maonyesho ya silaha usiku

Maonyesho ya silaha za Korea kaskazini APRIL 25 2022

Korea kaskazini imefanya maonyesho ya makombora yake ya masafa marefu katika gwaride la kijeshi lililofanyika usiku.

Wakati wa maonyesho hayo, kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un, ameapa kuendelea kutengeneza silaha za nuclear kwa mwendo wa kasi, kadri inavyowezekana.

Gwaride hilo kubwa la kijeshi lilifanyika mjini Pyongyang, katika bustan ya Kim Sung, na kuonyesha nguvu ya silaha za Korea kaskazini, ikiwemo makombora ya hali ya juu ya ICBM.

Kim Kong Un ameionya nchi yoyote itakayojaribu kuishambulia Korea kaskazini kwamba itaharibiwa kabisa.

Mwezi uliopita, Korea kaskazini ilifanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu kuwahi kufanyika tangu mwaka 2017.

Wataalam wanasema kwamba Korea kaskazini inatumia maonyesho ya silaha zake ili kuanzisha mazungumzo na Marekani kuhusu silaha za nuclear.