Ndege za Korea Kusini, za kutekeleza mashambulizi ya mabomu ziliruka angani huku magari ya kivita yakifyatua mizinga ya moshi hewani wakati wa mazoezi hayo ya kuvuka mito ya Namhan na Yeoju juu ya madaraja ya kuelekea, kusini mwa Seoul.
Korea Kusini na Marekani zimesema kwamba mazoezi hayo ni ya kujilinda na ni muhimu katika kuizuia Korea Kaskazini.
Kombora lililofyatuliwa na Korea kaskazini Oct 10, 2022
Kwa upande wake, Korea Kaskazini imejibu kwa kufyatua makombora kadhaa.
Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA, limeripoti kwamba jeshi la Korea Kaskazini limewaamuru wanajeshi wake kufyatua makombora kadhaa kutoka pwani ya Mashariki na Magharibi.
Jeshi la Korea Kaskazini limesema kwamba hatua hiyo ni ya kujibu mashambulizi ya roketi yaliyotekelezwa na Korea Kusini mara 10.
Majibizano ya kufyatua makombora yamejiri muda mfupi baada ya Korea Kaskazini kufyatua makombora 100 kuelekea baharini, na mengine 150 kutoka pwani yake ya Mashariki, Jumanne usiku.