Saudi Arabia imeandika historia leo Jumanne katika kombe la dunia linalofanyika Qatar, kwa kuishinda Argentina kwa mabao 2-1 katika mechi yao ya ufunguzi katika kundi C.
Mabao hayo mawaili yamefungwa na wachezaji Saleh Al Shehri na Salem Al-Dawsari.
Bao la Argentina limefungwa na nyota wao Lionel Messi kwa kupiga mkwaju wa penalti dakika ya 10 ya mchezo.