"Tunapaswa kujiandaa kwa kuzingatia kuwa vitadumu miaka kadhaa," Stoltenberg ameliambia gazeti la Ujerumani Bild am Sonntag. "Hatupaswi kuacha kuiunga mkono Ukraine, hata kama gharama ni kubwa, sio tu kwa msaada wa kijeshi, pia kwa sababu ya kupanda kwa bei ya nishati na chakuka."
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson, ambaye alifanya ziara mjini Kyiv siku ya Ijumaa na kuahidi mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine, alionya dhidi ya kuchoshwa na hali ya Ukraine wakati vita vya Ukraine vinaelekea kwenye mwezi wa nne siku zijazo.
Katika maoni yake yaliyochapishwa na gazeti la London Sunday Times, Johnson alisema ni kuhakikisha "Ukraine inapata silaha, vifaa, zana za kijeshi na mafunzo kwa haraka zaidi kuliko mvamizi."