Kandanda Wiki hii, Mei 03, 2013
Gonzalo Higuain kutoka Argentina, mchezaji wa Real Madrid akipiga mpira kichwa wakati wa duru ya pili ya nusu finali ya Champions League, Ulaya kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund mjini Madrid, Hispania, TJumanne, Aprili 30, 2013.
Fernando Torres wa Chelsea kulia, akijaribu kudhibiti mpira wakati mchezaji wa Basel Gaston Sauro kujaribu kumpokonya wakati wa duru ya pili ya nusu finali ya kombe la Europa katika uwanja michezo wa Chelsea Stamford Bridge mjini London, Alhamisi, Mei 2, 2013. (AP Photo/Kirst
Mchezaji wa Benfica, Rodrigo Lima, kutoka Brazil, kushoto, anapambana kuchukua mpira kutoka kwa mchezaji wa Fenerbahce, Joseph Yobo, kutoka Nigeria, wakati wa duru ya pili ya kombe la Europa Alhamisi, Mei 2 2013, mjini Lisbon.
Mchezaji wa timu ya Benfica Enzo Perez, kushoto, kutoka Argentina, akimenyana na golkipa wa timu ya Fenerbahce, Volkan Demirel, kulia, na Cristian, kutoka Brazil, wakati wa duru ya pili ya nusu finali ya kombe la Europa League mjini Lisbon, Alhamisi, Mei 2, 2013.
Cristiano Ronaldo kutoka Ureno akichezea Real Madrid wakati wa duru ya pili ya nusu finali ya Champions League kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund mjini Madrid, Hispania, Jumanne, April 30, 2013.
Ronaldinho wa Brazil akichezea Atletico Mineiro, kushoto, akipigania mpira na Wellington clabu ya Brazil ya Sao Paulo FC wakati wa mchuano wa kombe la Copa Libertadores mjini Sao Paulo, Brazil, Alhamisi, Mei 2, 2013.
Mchezaji wa Fenerbahce, Dirk Kuyt, kutoka Uholanzi akipiga mkwaju wa penalti ya kwanza katika duru ya pili ya nusu finali ya Europa League dhidi ya timu ya Benfica mjini Lisbon, Alhamisi, Mei 2, 2013.
David Beckham (kati) wa Paris St-Germain akishindana na Youssef Adnane (kushoto) wa Evian Thonon Gaillard na kupata kadi nyekundu wakati wa mchuano wa ligi ya juu ya Ufaransa mjini Annecy April. 28, 2013.
Wachezaji wa Dortmund Marco Reus and Marcel Schmelzer, wakisherehekea, baada ya kupata ushindi katika nusu finali ya Champions League na Real Madrid mjini Madrid, Hispania, Jumanne, Aprili 30, 2013.