Kabila aachilia wanaharakati wa kisiasa

Rais wa DRC, Jeseph Kabila, siku ya Jumatatu aliwaachilia wanaharakati wa kutetea demokrasia waliokamatwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wanaharakati wa kutetea demokrasia waliokamatwa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa wameachiliwa huru kufuatia msamaha wa rais kabila.

Wakati huohuo, vyama vikuu vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kikiwemo kile cha UDPS cha Etienne Tshisekedi nchini Kongo,vimeelezea msimamo wao wa kukataa mazungumzo ya kitaifa baada kukutana hii leo na maaskofu wa kanisa katoliki nchini humo. Upinzani umelazimisha kujiuzulu kwa msuluhishi wa mazungumzo hao ikiwa ni moja wapo ya masharti ya kushiriki kwenye mazungumzo.

Taarifa kamili na mwandishi wetu wa Kinshasa, saleh Mwanamilongo.

Your browser doesn’t support HTML5

Joseph Kabila releases political activists