Jinsi Krismasi inavyo sherehekewa nchi mbalimbali duniani

Mchungaji nchini Syria akiongoza ibada ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Maria huko mjini Diyarbakir, Uturuki, Disemba 25, 2018.

Prince Charles, Prince William, Duke wa Cambridge na Catherine, Duchess wa Cambridge akiwa na Prince Harry, Duke wa Sussex and Meghan, Duchess wa Sussex wakiwasili katika kanisa la mtakatifu Maria Magdalena kwa ibada ya Krismasi iliyoandaliwa kwa ajili ya familia ya kifalme Uingereza.

Wanajeshi wa Marekani na Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO ) wakiimba nyimbo za Krismasi wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Krismasi huko katika ofisi zake zinazo fanya usimamizi wa vikosi hivyo mjini Kabul, Afghanistan, Disemba 25, 2018.

Rais Donald Trump akiwasikiliza wanajeshi wa vikosi vitano vya jeshi wakati akifanya maongozi nao siku ya Krismas, Disemba 25, 2018, katika ofisi yake ndani ya White House. Wanajeshi hao wako nchini Guam, Qatar na Alaska  na makundi mawili yako Bahrain.

Watoto wa Kikristo nchini Pakistani wakiimba mwimbo katika kanisa la mtakatifu Patriki kabla ya sherehe za Krismasi mjini Karachi, Pakistani, Jumamosi, Disemba 22, 2018.

 

Kiongozi wa Kanisa la Katoliki Papa Francis akitoa ujumbe maalum wa Krismas kwa wakazi wa Vatican na watu wote duniani ikiwa ni salaam za heri ya Krismas kutoka dirisha kuu la Kanisa la Mtakatifu Petro huko mjini Vatican, Jumanne, Disemba. 25, 2018.

Waumini wa Palestina wakiwa katika paredi wakati wa maadhimisho ya Krismasi katika eneo la Manger Square nje ya Kanisa huko Bethlehem, katika eneo lilioko chini ya utawala wa Israeli Ukanda wa Magharibi, Disemba 24, 2018.

.Wachungaji wakihudhuria sherehe za Krismasi katika eneo la Manger Square nje ya Kanisa huko Bethlehem, katika eneo lilioko chini ya utawala wa Israeli Ukanda wa Magharibi , Disemba 24, 2018.

Katika ujumbe wa sikukuu ya Krismasi kwa wakazi wa Vatican na Ulimwengu mzima, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis awahamasisha watu wa mataifa yote na tamaduni mbalimbali kushikamana na kudumisha umoja.