Jeshi la Israel limesema leo Jumanne kuwa lilifanya mashambulizi ya anga ili kuharibu mitambo mitatu ya kurusha makombora ambayo ilitumika kutuma sehemu ya roketi 100 zilizorushwa kutoka Lebanon kuelekea Golan Heights inayokaliwa na Israel.
Ghasia za mpakani ni duru ya hivi karibuni ya mapigano ya mara kwa mara ambayo yameongeza wasiwasi wa kimataifa kuhusu kuenea kwa vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza hadi maeneo mengine katika eneo hilo.
Israel pia iliripoti Jumanne kufanya mashambulizi mapya ya anga katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza wakati ikisonga mbele na kampeni yake ya kulitokomeza kundi la wanamgambo wa Hamas.
Wakati Umoja wa Mataifa umeonya juu ya kuongezeka kwa mzozo wa chakula huko Gaza, meli iliyokuwa na tani 200 za misaada iliondoka Cyprus leo ikiwa njiani kupeleka misaada kwa njia ya bahari.