Jeshi la DRC latangaza ushindi dhidi ya waasi

Baadhi ya wanajeshi wa jeshi la DRC huko mashariki mwa Congo.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo - DRC limetangaza kuwa limepata ushindi dhidi ya kundi la waasi wa “Yakutumba Kivu Kusini” huko mashariki mwa Congo.

Kwa mujibu wa jeshi hilo vikosi vyake viliweza kumjeruhi kamanda wa waasi. Jeshi pia limesema limefanikiwa kuchukua silaha za kutosha pamoja na kuwakamata wapiganaji 120.

Wakati huo huo kamanda wa operesheni Kivu Kusini, Yave Philemo amewataka waasi waliobaki wasalimishe silaha zao hasa wale waliopo eneo la Ruzuzu linalopakana na mpaka wa Burundi.

Mwandishi wa VOA, Austere malivika anaripoti kutoka Goma huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Austere Malivika akiwa Goma, DRC