Israel imefungua njia kuingia Gaza

Mwanamme mpalestina akiwa amekaa kwenye nyumba yake ambayo imeharibiwa kutokana na mashambulizi ya makombora, Gaza.

Israel imesema kwamba inafungua tena njia zake za kuingia Gaza kwa muda mfupi, ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wakaazi wa sehemuhiyo.

Imesema kwamba itafungua njia hizo kwa ukamilifu baada ya hali ya utulivu kurejea.

Magari ya kusafirisha mafuta yameonekana yakiingia Gaza, kwa mara ya kwanza tangu sehemu hizo zilipofungwa wiki iliyopita, na kupelekea uhaba mkubwa wa mafuta.

Hatua hiyo inafuatia makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina na hivyo kumaliza mapigano ya siku tatu.

Ukanda wa Gaza pia le unakabiliwa na uhaba mkubwa wa umeme, na kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kinatarajiwa kuanza tena kufanya kazi baadaye hii leo.