Somalia yajitahidi kurudisha uhusiano wa kifedha

Shirika la fedha duniani, IMF, limesema kuwa Somalia imepiga hatua kubwa za kurejesha uhusiano na taasisi za kifedha za kimataifa.

IMF imesema jumatano kwamba ujumbe ulioongozwa na Rogerio Zandamela umekutana na mamlaka ya Somalia Machi 30 hadi Aprili 5, mjini Nairobi kuzungumzia program inayolenga sera za kuimarisha utawala na mikakati ya maendeleo kwenye sekta ya uchumi. Program ya aina hiyo huwa ni makubaliano yasio rasmi kati ya serikali na IMF yanayonuiya kusimamia utekelezwaji wa kuimarisha uchumi katika nchi.

Baada ya mkutano huo, Zandamela amesama kuwa juhudi za Somalia za kuimarisha serikali, jamii na uchumi zimeanza kuzaa matunda huku ukuaji wa uchumi ukikadiriwa kuwa asilimia 3.7 katika mwaka wa 2015. Hata hivyo amesema kuwa ukosefu wa usalama na uharibifu wa kivita vinaendelea kuathiri ushuru wa serikali na utoaji wa huduma muhimu kwa raia.